Red Cup ni neno la kiingereza lenye kumaanisha kikombe chekundu. Neno hili limetumika kukisi kikombe chekundu kinachotumika kuweka kimiminika hasa pombe.
Kiubunifu neno hili limetumika kwa kulenga taarifa na matukio yanayotokea katika tasnia ya burudani.
Red Cup ni kipindi cha runinga (Television) chenye kuhusisha taarifa za burudani. Kimaudhui imebeba dhima ya kuburudisha kupitia taarifa na matukio yanayotokea katika tasnia ya burudani kila inapoitwa siku. Maudhui ya kipindi cha Red Cup yamebeba dhima ya kutoa taarifa za burudani kwa kugusia mambo yanayoendelea katika kiwanda cha burudani Pamoja na kuhusisha mienendo ya maisha ya watu maarufu ndani na nje ya nchi.