Mchachuko

Karibu tuchachuke  uswahilini.

Neno MCHACHUKO ni neno la kiswahili lenye mnyumbulisho wa kitenzi chachuka ikimaanisha kitu chenye kuleta ukakasi mfano embe au mbilimbi. Kimaana, kipindi cha mchachuko ni ubunifu wa maneno wenye kulenga mazingira ya maisha yaliyochangamka na kubeba visa na matukio yenye kustaajabisha na kufurahisha.

Mchachuko ni kipindi cha runinga chenye mahadhi ya uswahili. Kimaudhui imebeba dhima ya kuelimisha na kuburudisha kupitia visa na matukio yanayotokea katika jamii zetu kila inapoitwa siku. Maudhui ya kipindi cha mchachuko yamebeba uhalisia wa maisha ya kundi la watu wanaoishi maisha ya ujamaa katika mazingira ya uswahilini.

#HUNuswahilini #HatunaBaya